Mkutano Mkuu wa marekebisho
ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika
salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku
wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC
Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai wapatao 1,560 kupitisha kipengele
hicho kipya kwa ajili ya maslahi na faida ya Wana Yanga kwani bila
kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha
katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa
usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi
utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji
amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi mapendekezo yao na kwa sasa
yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa
timu ya Taifa Tanzania kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini
Mama Fatma Karume aliongoza kikao cha waachama kilichomuomba Bw Manji
kuendelea na uongozi ambapo mwenyeikti alitoka nje na kamati yake ya
utendaji na pindi waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata
taratibu za kikatiba.
Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama umeazimia
kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu
wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza
kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF.
No comments:
Post a Comment