Saturday 7 June 2014

KIUNGO WA UJERUMANI MARCO REUS AUNGANA NA RIBBERY KURUDI NYUMBANI BAADA YA KUUMIA JANA

Down and out: Germany midfielder Marco Reus holds his left ankle in pain after injuring himself against Armenia
Hoi : Kiungo wa Ujerumani,  Marco Reus akiwa ameshika kifundo chake cha mguu wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Armenia
Ouch: Reus grimaces as he is helped to his feet by medical staff late in the first half
 Reus akitibiwa na madaktariwa timu ya taifa ya Ujerumani.
Expert care: Reus is taken off the pitch after receiving treatment from Germany's medical staff
 Reus akitolewa uwanjani kwa matibabu zaidi. 
 PIGO!,  Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa mabao 6-1 ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha kabla ya kuanza  kombe la dunia wiki ijayo.
Nyota huyo Borussia Dortmund alianguka chini baada ya kugongana na kiungo wa Armenia, Artur Yedigaryan na kuambulia kuumia na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wa Ujerumani na benchi zima la ufundi.
Reus aliachwa amelala chini kwa maumivu makali na kupatiwa matibabu uwanjani kabla ya kutolewa katika mchezo huo kabla ya muda wa mapumziko.
Nyota huyo mwenye miaka 25 aliripotiwa kushindwa hata kuvaa kiatu katika mguu wake wa kushoto na imeelezwa kuwa alipelekwa moja kwa moja hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina.
 
Joachim Low anajiandaa kucheza na Ureno juni 16 katika mechi ya ufunguzi, na inawezekana Reus akazikosa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Akizungumza baada ya mechi, Low alisema: “Tuna matarajio kuwa atapona. Lakini inaonekana kuwa mbaya sana. Tunaweza kumuita mchezaji mwingine saa 24 kabla ya mchezo wa kwanza”

No comments:

Post a Comment