Wachezaji 26 wa
Taifa Stars wanaingia kambini Jumatatu (Juni 23 mwaka huu) kwa ajili ya safari
ya Gaborone, Botswana.
Kwa mujibu
wa Kocha Msaidizi wa timu hiyo Salum Mayanga, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti
katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa safari hiyo
inayotarajiwa kuwa Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji
hao ni wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula,
Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason,
Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni
Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna
Chanongo, Himid Mao, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano,
Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
No comments:
Post a Comment