DEWJI (KATIKA) AKIWA NA KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA, MILOVAN CIRKOVIC (KULIA), MWINGINE NI MWANACHAMA WA SIMBA |
Mfadhili wa
zamani wa Simba, Azim Dewji amewaita waandishi wa habari.
Ingawa bado
hajaweka wazi anataka kuzungumzia nini, lakini SALEHJEMBE imeng’amua Dewji
anataka kuzungumzia suala linalohusu mgombea wa urais aliyeengulia baada ya
kugundulika uanachana wake una walakini, Michael Wambura na Rais wa TFF, Jamal
Malinzi.
“Kweli Dewji
atakuwa na kikao saa 5 asubuhi, nafikiri ana kitu kuhusiana na Wambura na
Malinzi.
“Lakini
sijajua ni nini hasa, lakini Dewji atazungumza mwenyewe Jumapili, vizuri
ukaenda na kujua,” alisema mpasha habari.
Tayari
Wambura amekata rufaa TFF kupinga kuondolewa kwenye uchaguzi na kamati ya
uchaguzi ya Dkt Damas Daniel Ndumbaro.
CHANZO; Saleh Ally blog
No comments:
Post a Comment