SIMBA na Yanga kila moja itanunua wachezaji
wawili wa kigeni nje ya nchi. Yanga inamfikiria straika wa Uganda
anayecheza Gor Mahia,Dan Sserunkuma na imeshazungumza nae.
Lakini Simba nayo kocha wake, Zdravko Logarusic amezungumza na wachezaji watatu wa Kenya akiwemo, Rama Salim wa Gor Mahia.
Ingawa Mwanaspoti linajua kwamba Simba wamezungumza na wachezaji wawili wa Uganda na muda wowote wataletwa nchini.
Lakini AFC Leopards ya Kenya imeingia kwenye kinyang’anyiro na kusaka saini za Danny na Rama ambao wote wana mikataba.
“Tunawasaka wachezaji wanaoweza kujaza nafasi ya
Allan Wanga na tunahisi kuwa Sserunkuma ni mmoja wao. Rama vile vile ni
mzuri na ushirikiano wake na Sserunukma unaweza kutufaa,” alisema
Patrick Ngaira ambaye Mwenyekiti msaidizi wa AFC.
No comments:
Post a Comment