Thursday 19 June 2014

KUMBE KIUNGO WA IVORY COAST SEREY DIE ALIFIWA NA BABA YAKE SAA 2 KABLA YA MECHI/ SEREY DIE LOST HIS FATHER 2 HRS BEFORE KICK-OFF

 Kilio cha kiungo wa Ivory Coast, Serey Die wakati wimbo wa taifa lake ukipigwa katika mechi dhidi ya Coloimbia kiliwashangaza wengi.
Wako waliodhani ni uzalendo tu, lakini wengine walifikiri ni tatizo lakini ukweli ni kwamba Die alifiwa na baba yake mzazi saa mbili kabla ya mechi.
Die ,29, aliangua kilio kwa nguvu hadi wenzake wakalazimika kumbembeleza.
Lakini baadaye akapata gundu tena baada ya kutoa ‘boko’ lililozaa bao la pili kwa Colombia ambayo iliilaza Ivory Coast kwa mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment