Wednesday, 18 February 2015

MWAKALEBELA AULA, RAIS KIKWETE AMTEUA KUWA MKUU WA WILAYA

Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.


Kati ya hao ni Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Wilfred Mwakalebela ambaye ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mwakalebela ameula baada ya Rais Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

No comments:

Post a Comment