Mshambuliaji nyota wa Brazil,
Neymar jana aliumia mazoezini na kuzua hofu kubwa.
Wabrazil ndiyo wanamuweka
mbele kama tegemeo namba moja, Neymar aliumia enka na baada ya muda aliweza
kuendelea na mazoezi lakini baada ya kupatiwa tiba kwa muda kadhaa.
Hali hiyo imezua hofu kama
kweli Neymar atakuwa katika kiwango safi katika mechi ya ufunguzi dhidi ya
Croatia.
Neymar ndiye nyota ambaye
Brazil wanaamini atakuwa shujaa wao katika michuano ya Kombe la Dunia inayoanza
keshokutwa.
Lakini hakuna taarifa
yoyote kutoka kwenye kikosi hicho iliyosema anaweza asiwe katika kiwango
kizuri.
No comments:
Post a Comment