Thursday 11 June 2015

Exclusive:Simba yatoa tamko kuhusu Singano

Hata hivyo Klabu itakuwa tayari kufanya naye mazungumzo pindi muda muafaka utakapofika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mikataba
PAMOJA na Shirkisho la soka Tanzania TFF, kutoa ufafanuzi kuhusiana na swala la winga Ramadhani Singano ‘Messi’ mvutano umezidi kuendelea kwa pande zote mbili huku Rais wa klabu ya Simba kwa kushirikiana na kamati ya utendani ya klabu hiyo wakitoa kauli yao le
Goal imezungumza na Rais wa Simba Evans Aveva na haya hapa ndiyo maazimio yao kufuatia mchezaji huyo kuvunja makubaliano yaliyoamuliwa na TFF.
Kikao cha kamati ya utendaji ya club ya simba kilichokutana jana tarehe 10/06/2015, pamoja na mambo mengine kilijadili suala la mchezaji wa Simba Ramadhan Yahya Singano na kuamua yafuatayo:
Kwakuwa mchezaji Ramadhan Singano alivunja makubaliano yaliyoamuliwa katika kikao cha pamoja kati ya club ya Simba, mchezaji mwenyewe, sputanza na secretarieti ya shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) ya kutozungumzia yaliyojadiliwa na kupendekezwa kwenye kikao kwa kuyazungumza kwenye vyombo vya habari kwa kusema yeye ni mchezaji huru,
Klabu ya simba imeamua kutokufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwa sasa kwa kuwa bado ina mkataba naye ambao utaisha 01/07/2016.
Hata hivyo Klabu itakuwa tayari kufanya naye mazungumzo pindi muda muafaka utakapofika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mikataba.
Ni matarajio yetu mchezaji Singano ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia upo TFF na kwenye mtandao TMS.

No comments:

Post a Comment