Mgombea wa nafasi
ya Urais ya Simba aliyeenguliwa, Michael Wambura, amekata rufaa tena.
Kamati ya
uchaguzi ya Simba, ilitangaza kumuondoa Wambura kwa mara ya pili kwenye
uchaguzi huo baada ya kupiga kampeni kabla ya muda.
Lakini Wambura
amewasilisha rufaa hiyo leo na imeelezwa tayari imepangiwa siku.
Awali Rais wa
TFF, Jamal Malinzi alitaka Simba kuunda kamati ya maadili, lakini safari hii
kamati yake ya nidhamu imepokea rufaa ya Wambura na itasikilizwa mara moja!
Kamati ya rufaa
ndiyo iliyomrudisha Wambura kugombea baada ya kuwa ametemwa na kamati ya
uchaguzi.
No comments:
Post a Comment