Saturday, 4 April 2015

MASHABIKI WA SIMBA UKAWA WAPATA AJALI MOROGORO

IMG-20150403-WA0109Habari mbaya na ya kusikitisha kuhusu kikundi cha ushangiliaji cha tawi la Simba la Mpira na Maendeleo maarufu kwa jina la Simba Ukawa iliyotokea leo mjini Morogoro wakielekea mjini Shinyanga kuisapoti timu yao inayocheza mechi ya ligi kuu kesho dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa mpya na za uhakika zinasema watu saba (7) akiwemo kiongozi wa Simba Ukawa, Mohammed Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ wamefariki dunia na watu 15 wapo mahututi.
Ajali hiyo imetokea eneo la Mvomero ikihusisha basi dogo aina ya Toyota Costa lililopinduka na kuacha njia. Polisi bado hawajatoa tamko rasmi.
Waliotangulia mbele ya haki mpaka sasa ni:
Waluya, Rehema, Ali Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ Wabi na dereva wa gari Abdallah Fundi.

No comments:

Post a Comment