KLABU ya Yanga inatarajiwa kukabidhiwa kombe lake la
ubingwa wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara Mei 6 kwenye uwanja wa taifa
Dar es Salaam
KLABU ya Yanga inatarajiwa kukabidhiwa kombe lake la ubingwa wa Ligi
ya Vodacom Tanzania bara Mei 6 kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam
baada ya kumalizika pambano kati yao na waliokuwa mabingwa watetezi Azam
FC.
Waziri wa michezo Dr Fennela Mkangara ndiye atakaye kabidhi kombe
hilo la 25 kwa mabingwao hao wa Kihistoria baada ya jana jumatatu
kuifunga Polisi Moro mabao 4-1, na kufikisha pointi 55 ambazo hazitaweza
kufikiwa na timu nyingine inayoshiriki ligi hiyo msimu huu.
Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi ameiambia Goal
siku hiyo itakuwa rasmi kukabidhi baadhi ya zawadi kwa washindi wa ligi
hiyo na ndiyo sababu wakamteuwa waziri kuwa mgeni rasmi.
“Kwanza nampongeza Mwenyekiti wa klabu ya, Yusuf Manji kwa timu yake
kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Vodacom msimu wa 2014/2015 , kwasababusiyo
kazi nyepesi na jambo muhimu sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili
ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.
No comments:
Post a Comment