Monday 13 April 2015

Match Report:Yanga 3 – 1 Mbeya City, Yanga yaunyemelea ubingwa

Idadi ya mabao iliyoyapata Yanga leo inafanana na mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya ambapo ilishinda mabao 3-1
KLABU ya YANGA jioni ya leo imeendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi za Ligi ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuifunga timu ya Mbeya City mabao 3-1.
Ushindi wa leo unaifanya Yanga kuhitaji pointi sita katika michezo mitano iliyobakiwa nayo ili kuivua ubingwa Azam FC, ambayo kwa sasa ipo nyuma kwa nane.
Idadi ya mabao iliyoyapata Yanga leo inafanana na mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Sokoine Mbeya ambapo ilishinda mabao 3-1.
Ushindi wa leo ni watano mfululizo kwa kikosi cha Yanga ambacho mara ya mwisho kilifungwa kwenye mechi za ligi ya Vodacom ilikuwa ni Machi ilipopoteza kwa bao 1-0 dhid ya Simba uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Yanga iliuanza wa leo kwa kasi huku washambuliaji wake wakionekana wenye uchu wa mabao kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita walipoifunga Coastal Union ya Tanga mabao 8-0. Mshambuliaji raia wa Liberia alikuwa kwenye kiwango cha juu leo aliifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 18 akiunganisha pasi ya Amissi Tambwe.
Hilo ni bao la pili kwa Sherman aliyesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu akitokea Citinkaya TSK ya Cyprus, baada ya Jumatano kufunga bao lake la kwanza kwenye ushindi wa 8-0.
Bao hilo liliongeza kasi ya mchezo kwa timu zote mbili lakini kiungo mkabaji Salum Telela, aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 37 baada ya kupiga shuti kali lilowababatiza mabeki wa Mbeya City na kumpoteza kipa Hanington Kalyesubula. Mbeya City ambao Jumatano iliyopita walitoka sare ya 1-1 na Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex, walikuja juu na kufanikiwa kupata bao dakika ya 39, akiunganisha pasi ya Raphael Alpha.

Dakika nne baada ya kuanza kipindi cha pili nahodha wa Yanga, Nadir Haroub aliifungia timu yake bao la tatu akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliokuwa umepigwa na Haruna Niyonzima dakika ya 49. Mbeya City ambayo inashiriki msimu wapili mfululizo ligi ya Vodacom Tanzania bara ililazimika kucheza pungufu baada ya mwamuzi Mathew Akrama wa Mwanza kumtoa kwa kadi nyekundu Felix kwa kumchezea rafu Telela katika dakika ya 53.

Rafu hiyo ilimfanya Telela kushindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Hassan Dilunga katika dakika ya 61.

Dakika ya 21, Sherman alikosa bao baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa wa Mbeya City, Kalyesubula. Paul Nonga wa Mbeya City alikosa bao katika dakika ya 32 baada ya shuti lake kupaa juu. Amissi Tambwe alikosa bao katika dakika ya 42 baada ya shuti lake kutoka nje.

No comments:

Post a Comment