Kwa ushindi huo Simba imeendelea kubaki nafasi ya
tatu ikifikisha pointi 41 huku Yanga ikibaki kileleni kwa pointi zake 52
na Azam nafasi ya pili na pointi 45
SIMBA leo imeendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya kupata
ushindi wa pili mfululizo kwa kuifunga Ndanda FC, ya Mtwara mabao 3-0.
Ushindi huo umeifanya Simba kuungana na Azam FC, kupigania kumaliza
nafasi ya pili msimu huu ili moja wapo iungane na Yanga kwenye
kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa 2016.
Kwa ushindi huo Simba imeendelea kubaki nafasi ya tatu ikifikisha
pointi 41 huku Yanga ikibaki kileleni kwa pointi zake 52 na Azam nafasi
ya pili na pointi 45.
Ikicheza mbele ya mashabiki wake wacheche waliojitokeza leo
kuishangilia Simba ilianza kuhesabu bao lake kwa kwanza dakika ya tisa
lililofungwa kwa shuti la mbali na kiungo Jonas Mkude.
Kuinhia kwa bao hilo kulionekana kuwaongezea kasi vijana wa kocha
Goran Kopunovic na dakika ya 10 mshambuliaji hatari wa Simba Emmanuel
Okwi aliangushwa ndani ya eneo la hatari na kuwa penalty ambayo Ibrahim
Ajibu alikosa kwa shuti lake kupaa juu.
Ramadhani Singano alisawazisha makosa ya Ajibu dakika ya 15, baada ya
kufunga bao la pili akitumia makosa ya kipa wa Ndanda FC Salehe
Malande, aliyekuwa akiuchezea mpira kwenye eneo la hatari na kuanguka
chini na mfungaji kufunga kirahisi.
Ndanda FC inayoshika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na
pointi 25 ilijitahidi kutaka kupata angalau bao moja baada ya dakika ya
19 Kigi Makasi, kupiga mpira wa faul ambao ulipanguliwa kiufundi na kipa
Ivo Mapunda na kuwa kona ambayo haikuwa na matunda.
Jitihada za wachezaji wa Ndanda FC kutaka kwenda mapumziko walau na
bao moja ziliingia dosari dakika ya 21 baada ya kiungo Said Ndemla
kuifungia Simba bao la tatu kwa shuti kali akiunganisha krosi ya
Ramadhani Singano.
Kipindi cha pili, Ndanda FC ilicheza vizuri zaidi na kufanya
mashambulizi ya nguvu langoni mwa wapinzani wao na kupata bao
lililofungwa na Stamili Mbonde katika dakika ya 50, lakini mwamuzi
Kingstone Liza, alilikataa kwa sababu mfungaji alikuwa ameotea.
Mshambuliaji wa Ndanda FC Gideon Benson alifanya na kuonyesha kiwango
cha juu kutokana na kuwasumbua mabeki wa Simba lakini alikosa msaada
baada ya Kigi Makasi kurudi kucheza nyuma.
Kocha Goran Kopunovic amefuraishwa na matokeo hayo na kusema
wataendelea kupambana kupata pointi sita katika mechi zao mbili zilizo
baki na siku ya mwisho watajua wapo nafasi gani.
No comments:
Post a Comment