Wednesday, 8 April 2015

TFF yaiamuru Simba imalizane na Tambwe.

TFF limeiandikia barua Klabu ya Simba likiitaka kumlipa mshambuliaji Amisi Tambwe wa Yanga fedha zake za kuvunja mkataba milioni 20
SHIRIKISHO la Soka Tanzania TFF, limeiandikia barua Klabu ya Simba likiitaka kumlipa mshambuliaji Amisi Tambwe wa Yanga fedha zake za kuvunja mkataba milioni 20.
Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa ameiambia Goal kuwa wamewapa Simba nafasi hiyo endapo watashindwa kuitumia watawachukulia hatua zaidi
“Hatuwezi kuzungumzia swala moja kila siku hii ni mara ya pili Tambwe anatuletea mashtaka na sisi tungependa wamalizane kwa amani kabla hatujaamua kwenda mbele zaidi,”mesema Mwesigwa.
Katibu Mkuu wa Simba Stiven Ally amekiri kupokea barua hiyo kutoka TFF, na kusema ataiwasilisha kwa viongozi wa juu ambao ndiyo wenye mamlaka ya kuijibu.

No comments:

Post a Comment