MECHI ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil itapigwa kwenye Uwanja wa Maracana, Julai 13, 2014.
Lakini, uwanja huo wa kihistoria ni moja ya
viwanja 12 katika miji 12 tofauti itakayotumika kwa ajili ya fainali
hizo za soka zitakazoshuhudia timu 32 zikimsaka mwamba mmoja wa Dunia.
Makala hii inazungumzia viwanja vyote 12
vitakavyotumika kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia ambazo zitaanza
rasmi Juni 12 mwakani kwa mechi ya Brazil dhidi ya Croatia itakayopigwa
kwenye Uwanja wa Arena Corinthians jijini Sao Paulo.
Uwanja: Maracana
Jiji: Rio de Janeiro
Uwezo: Watazamaji 73,531
Klabu zinazoutumia: Fluminense FC na CR Flamengo
Rio de Janeiro ni jiji la aina yake Brazil na
hakika Uwanja wa Maracana una historia ya kipekee katika soka la Dunia.
Maracana ilijengwa upya kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Ulifunguliwa Juni mwaka huu kwa mechi ya kirafiki kati ya Brazil na
England.
Ndiyo uwanja utakaotumika kwa fainali Julai 13
mwakani, mandhari yake nzuri ndicho kitu kinachovutia zaidi kwenye mji
huo kutokana na kuwa na fukwe safi na vivutio vingine vya kitalii kama
Mlima wa Sugar Loaf na Sanamu ya Christ the Redeemer.
Maracana ulitumiwa kwenye mechi ya fainali ya
Kombe la Dunia 1930, ambapo mashabiki 200,000 waliingia na kuishuhudia
Uruguay ikiichapa Brazil
Mechi zitakazochezwa:
Juni 15, 2014 - Argentina v Bosnia&Herzegovina - Kundi F
Juni 18, 2014 - Hispania v Chile Juni 22, 2014 - Ubelgiji v
Russia Juni 25, 2014 - Ecuador v Ufaransa Juni 28, 2014 - Mshindi Kundi C
v Mshindi wa pili Kundi D
Julai 4, 2014 - Robo fainali
Julai 13, 2014- Fainali
Uwanja: Arena Corinthians
Jiji: Sao Paulo
Uwezo: Watazamaji 65,000
Klabu zinazoutumia: Corinthians
Kumeibuka wasiwasi mkubwa juu ya uwanja huo kama
utaweza kutumika kwa mechi ya ufunguzi baada ya moja ya vyuma vya jukwaa
kuporomoka na kusababisha vifo vya wafanyakazi wawili. Sao Paulo ni mji
unaosifika kuwa ndipo soka ilipozaliwa kwa nchi ya Brazil, lakini hali
ya hewa yake imekuwa tatizo kidogo.
Mji huo wa Kusini Mashariki unafahamika kama Terra da Garoa kutokana na mvua kunyesha mara kwa mara.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 12, 2014 - Brazil v Croatia Juni 19, 2014 - Uruguay v England
Juni 23, 2014 - Uholanzi v Chile Juni 26, 2014 -
Korea Kusini v Ubelgiji Julai 1, 2014 - Mshindi Kundi F v Mshindi wa
pili Kundi E
Julai 9, 2014 - Nusu fainali
Uwanja: Estadio Nacional Mane Garrincha
Jiji: Brasilia
Uwezo: Watazamaji 68,009
Jina la uwanja huo limetokana na nyota wa zamani
wa Botafogo na Brazil, Garrincha, ambaye alikuwa mmoja wa wanasoka
mahiri kabisa nchini huko katika miaka ya 1950 na 1960.
Uwanja huo mpya ulitumika kwenye mechi ya ufunguzi
ya Kombe la Mabara. Brasilia ni jiji lenye wasanifu wengi wa
miundombinu. Ulianza kutambulika kama mji mkuu wa Brazil badala ya Rio
de Janeiro mwaka 1960.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 15, 2014 - Usiswi v Ecuador
Juni 19, 2014 - Colombia v Ivory Coast
Juni 23, 2014 - Cameroon v Brazil Juni 26, 2014 - Ureno v Ghana Juni 30, 2014 -
Mshindi Kundi E v Mshindi wa pili Kundi F
Julai 5, 2014 - Robo fainali
Julai 12, 2014 - Mechi ya mshindi wa tatu
Uwanja: Estadio Castelao
Jiji: Fortaleza
Uwezo: Watazamaji 58,704
Klabu zinazoutumia: Ceara SC na Ferroviario AC
Uwanja huo ambao utatumika kwa mechi ya pili ya
Brazil ya hatua ya makundi umeandaliwa kwa kipindi cha miaka miwili kwa
ajili ya kutumika kwa fainali hizo za Kombe la Dunia. Fortaleza, mji
uliopo Kaskazini Mashariki mwa Brazil ni mjii wa mkuu wa kitongoji cha
Ceara.
Fortaleza ni maarufu kwa utalii, fukwe nzuri na vyakula vya aina yake na unatajwa kuwa na hali ya Kitropiki.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 14, 2014 - Uruguay v Costa Rica Juni 17, 2014
- Brazil v Mexico Juni 23, 2014 - Ujerumani v Ghana Juni 24, 2014 -
Ugiriki v Ivory Coast
Juni 29, 2014
Mshindi Kundi B v mshindi wa pili Kundi A
Julai 4, 2014 - Robo fainali
Uwanja: Estadio Mineirao
Jiji: Belo Horizonte
Uwezo: 57,483
Klabu inyoutumia: Cruzeiro Esporte Clube
Ni uwanja utakaotumika kwa mechi ya nusu fainali
na ni uwanja uliokamilika kwa wakati mara tu Brazil ilipotajwa kuwa
mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2014.
Straika wa zamani wa Brazil, Ronaldo aling’ara
kwenye uwanja huo wa Mineirao wakati alipoanza soka lake katika Klabu ya
Cruzeiro.
Upo umbali wa mwendo wa saa moja kutoka Rio de Janeiro na ni mji usio na gharama kubwa kwa mashabiki wa kigeni.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 14, 2014 - Colombia v Ugiriki Juni 17, 2014 -
Ubelgiji v Algeria Juni 21, 2014 - Argentina v Iran Juni 24, 2014 -
Costa Rica v England
Juni 28, 2014 - Mshindi Kundi A v Mshindi wa pili Kundi B
Julai 8, 2014 - Nusu fainali
Uwanja: Estadio Beira-Rio
Jiji: Porto Alegre
Uwezo: 48,849)
Klabu zinazoutumia: Sport Club Internacional
Uwanja huo upo kando ya Mto Guaiba. Unatumika kama
uwanja wa nyumbani wa klabu mbili maarufu za Internacional na majirani
zao Gremio. Porto Alegre ni mji wenye mvua kipindi cha Juni na Julai na
visiwa na kimojawapo ni Lago de Patos kilichozungukwa na miti karibu
milioni moja.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 15, 2014 - Ufaransa v Honduras Juni 18, 2014 -
Australia v Uholanzi Juni 22, 2014 - Korea Kusini v Algeria Juni 25,
2014 - Nigeria v Argentina
Juni 30, 2014 - Mshindi
Kundi G v Mshindi wa pili
Uwanja: Arena Pernambuco
Jiji: Recife
Uwezo: Watazamaji 44,248
Klabu zinazoutumia: Nautico
Jiji la Recife, lipo kwenye Pwani ya Kaskazini Mashariki ya
Brazil, ulitumika mara ya mwisho katika mechi ya Kombe la Dunia 1950.
Kwa sasa umejengwa upya na unatumiwa na klabu tatu zenye historia ya
kipekee Brazil za Nautico, Santa Cruz na Sport. Wakazi wake ni vichaa wa
soka.
Recife ni mji mkuu wa Pernambuco ni muhimu sana kwa uchumi wa Brazil.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 14, 2014 - Ivory Coast v Japan Juni 20, 2014 - Italia v Costa Rica
Juni 23, 2014 - Croatia v Mexico
Juni 26, 2014 - Marekani v Ujerumani
Juni 29, 2014 - Mshindi Kundi D v Mshindi wa pili Kundi C
Uwanja: Arena Fonte Nova
Jiji: Salvador
Uwezo: Watazamaji 52,048
Klabu zinazoutumia: EC Bahia na EC Vitoria
Uwanja huo utashuhudia mechi sita kwenye fainali
hizo. Waandaaji wanasema uwanja huo mpya umejengwa kisasa na una
migahawa, makumbusho za soka, maduka, hoteli na kumbi za sherehe.
Umerekebishwa upya baada ya paa lake kubomolewa na mvua Mei mwaka huu, lakini hakukuwa na majeruhi yeyote aliyeripotiwa.
Salvador ni mji uliopo Kaskazini mwa Brazil na ndiyo uliokuwa mji mkuu wa kwanza wa nchi hiyo.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 13, 2014 - Hispania v Uholanzi Juni 16, 2014 -
Ujerumani v Ureno Juni 20, 2014 - Uswisi v Ufaransa Juni 25, 2014 -
Bosnia&H v Iran
Julai 1, 2014 - Mshindi
Kundi H v Mshindi wa pili
Julai 5, 2014 - Robo fainali
Uwanja: Arena Pantanal
Jiji: Cuiaba
Uwezo: Watazamaji 42,968
Klabu zinazoutumia: Cuiaba EC na Mixto EC
Uwanja huo uliboreshwa kwa ajili ya fainali za
Kombe la Dunia na utatumika kwa ajili ya mechi nne. Uwanja huo upo
kwenye mji wa Cuiaba uliopo Magharibi mwa Brazil, Kusini mwa misitu ya
Amazon.
Mji huo unafahamika kama ‘Green City’ na ni maarufu kwa utalii
licha ya kwamba kwa kipindi cha Juni hadi Julai hali ya hewa inakuwa
tatizo kutokana na joto kufikia nyuzi 40.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 13, 2014 - Chile v Australia
Juni 17, 2014 - Russia v Korea Kusini
Juni 21, 2014 - Nigeria v Bosnia&He
Juni 24, 2014 - Japan v Colombia
Uwanja: Arena Amazonia
Jiji: Manaus
Uwezo: Watazamaji 42,374
Kama jina la uwanja huo linavyosomeka, Manaus ipo
katikati ya misitu ya Amazon. Manaus si mahali pazuri sana kwa soka,
lakini waandaaji wa Kombe la Dunia waliamua michuano hiyo ifanyike kila
kona ya nchi ya Brazil licha ya kwamba uwanja huo unaweza kuwa bustani
ya wanyama michuano itakapokwisha.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 14, 2014 - England v Italia Juni 18, 2014 -
Cameroon v Croatia Juni 22, 2014 - Marekani v Ureno Juni 25, 2014 -
Honduras v Uswisi
Uwanja: Estadio das Dunas
Jiji: Natal
Uwezo: Watazamaji 42,086
Klabu zinazoutumia: America FC
Uwanja huo umemalizika kujengwa kwa ajili ya Kombe
la Dunia. Estadio das Dunas utatumika kwa mechi nne za makundi katika
fainali hizo. Natal ni mji unaofahamika kama Cidade do Sol (Sun City)
kwa sababu umekuwa na joto linalokaribia nyuzi 28. Fukwe zilizopo
Kaskazini Mashariki mwa jiji hilo zinaifanya jiji hilo lizidi kupendeza.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 13, 2014 - Mexico v Cameroon
Juni 16, 2014 - Ghana v Marekani
Juni 19, 2014 - Japan v Ugiriki
Juni 24, 2014 - Italia v Uruguay
Uwanja: Arena da Baixada
Jiji: Curitiba
Uwezo: Watazamaji 41,456
Klabu zinazoutumia: Atletico Paranaense
Uwanja huo wa Arena da Baixada kwa mara ya kwanza
ulijengwa 1914, lakini ulifanyiwa ukarabati mwaka 1999 na ulirekebishwa
zaidi baada ya Brazil kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la
Dunia 2014.
Curitiba ni mji wa aina yake ndani ya Brazil na
unatajwa kuwa na uchumi mkubwa. Hali yake ya hewa inafanana na Rio de
Janeiro na Belo Horizonte.
Mechi zitakazochezwa:
Juni 16, 2014 -
Iran v Nigeria
Juni 20, 2014 -
Honduras v Ecuador
Juni 23, 2014 - Australia v Hispania
Juni 26, 2014
Algeria v Russia
No comments:
Post a Comment