Friday, 6 June 2014

BIN SLUM TYRES YAINGIA MKATABA NA MBEYA CITY, YAMWAGA MILIONI 360

MOHAMMED BIN SLUM (KULIA) NA MWANASHERIA WA MBEYA CITY WAKIONYESHA MKATABA HUO.

Kampuni maarufu nchini katika uuzaji wa matairi, betri, pikipiki na nyinginezo ya Bin Slum Tyres Limited, imeingia mkataba wa udhamini na klabu ya Mbeya City kwa miaka miwili.

Bin Slum Tyres Limited imeonyesha kweli imepania kuingia kwenye udau wa kuchangia maendeleo ya soka nchini baada ya kumwaga Sh milioni 360 kwa miaka hiyo miwili.
Mkataba huo na Wagonga nyundo wa jiji la Mbeya umesainiwa leo jijini Dar es Salaam kwenye makao makuu ya Bin Slum Tyres Limited.
Kutokana na mkataba huo, Mbeya City watakuwa wakitupia uzi wa RB Battery, moja ya betri bora za magari nchini zinazosambazwa na kampuni hiyo.
Awali Bin Slum Tyres Limited ilikuwa ikiidhamini Coastal Union ya Tanga ambayo hivi karibuni ilianzisha harambee ya kusaka fedha kujiandaa na msimu mpya wa 2014-15.
Mmoja wa wakurugenzi wa Bin Slum Tyres Limited, Mohammed Bin Slum ndiye aliyeingia mkataba huo na mwanasheria wa Mbeya City.
Bin Slum Tyres Limited inakuwa moja ya kampuni zinazotia chachu katika maendeleo ya mchezo wa soka nchini.

No comments:

Post a Comment