TAIFA STARS |
Kiingilio cha chini cha
mechi ya kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames)
itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh.
5,000.
Washabiki watakaolipa
kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu
na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa
VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Mechi hiyo itaanza saa 11
kamili jioni ili kutoa fursa kwa washabiki wengi zaidi kuishuhudia kwa vile
itakuwa ni siku ya kazi.
Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo ya mechi
kutoka Tukuyu mkoani Mbeya ambapo imepiga kambi yake chini ya Kocha Mholanzi
Mart Nooij.
Malawi (Flames) inayonolewa
na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa ajili ya mechi
hiyo inayotumiwa na timu zote kama maandalizi ya mwisho kwa ajili mechi za
mchujo za Kombe la Afrika (AFCON).
Wakati Stars kwenye mechi za AFCON itarudiana na
Zimbabwe jijini Harare, Flames nayo itakuwa ugenini N’djamena kukabili Chad
No comments:
Post a Comment