Bao pekee la Mbwana Samatta katika dakika ya 62
limeipa ushindi TP Mazembe dhidi Vita Club.
Vita ambao ni wapinzani wakubwa wa TP Mazembe wamelala kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi, timu hizo zikiwa zinatokea kundi A.Mechi hiyo mjini Lubumbashi ilikuwa na upinzani mkali.
Kawaida Vita kutoka Kinshasa imekuwa na
upinzani wa juu dhidi ya Mazembe.
Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu alikuwa
kwenye benchi katika mechi hiyo.
Ulimwengu ni kati ya wachezaji wachache makinda
ambao wamepata nafasi ya kucheza kwenye timu yenye ushindani kama Mazembe.
Kwa matokeo hayo, kila timu katika kundi lao
inakuwa imepoteza mchezo mmoja kwa kuwa katika mechi ya mwisho Mazembe
ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi Al Hilal ya Sudan ambayo nayo imelala 2-1 kwa
Waarabu wa Misri, Zamalek.
No comments:
Post a Comment