CRISTIANO
Ronaldo na Gareth Bale wameongoza sherehe za ubingwa wakati Real Madrid
wakipita mitaa ya mji mkuu wa Hispania, Madrid, wakishangilia kunyakua
ubingwa wa UEFA kwa kuwafunga mabao 4-1 wapinzani wao Atletico Madrid
katika mchezo wa fainali jana usiku mjiji Lisbon
Wachezaji
wa Real wamesherehekea na mashabiki wao mapema leo asubuhi wakiwa
katika basi la wazi mjini Madrid ikiwa zimepita saa kadhaa tangu
wachukue ndoo ndani ya dakika za nyongeza.
Wachezaji
wa Carlo Ancelotti baada ya kumalizika kwa mechi mjini Lisbon
walisafiri moja kwa moja kurudi Madrid na kushangilia usiku kucha.
Ukiongoza sherehe: Cristiano Ronaldo akiimba wimbo wakati wakiwa katika basi la wazi.
Mabingwa: Wachezaji wa Madrid wakirudi Madrid kushangilia na mashabiki wao mapema leo asubuhi.
Furaha ya kweli: Wachezaji wa Real wakishangilia na mashabiki wao maeneo ya Cibeles Square mjini Madrid baada ya kushinda Lisbon
Nyomi: Maelfu ya mashabiki wakiwa wamefurika katika mitaa ya Madrid mapema asubuhi kuwapokea mashujaa wao.
Sergio Ramos, Pepe, Ronaldo, Jese na Fabio Coentrao wakishangilia
Amezama katika busu: Nahodha Iker Casillas akilibusu kombe mbele ya maelfu ya mashabiki wa Real Madrid leo mjini Madrid
Mtaalam: Carlo Ancelotti akishangilia na kombe
Wapendanao: Ronaldo akishangilia ubingwa na demu wake Shayk, huku akiwa na medali yake
Angel
di Maria (picha ya juu) na Marcelo (picha ya chini) wakishangilia
ubingwa na wake zao wakati wakiwa ndani ya ndege kurudi mjini Madrid
No comments:
Post a Comment