Thursday, 19 February 2015

Rekodi 8 kubwa alizoweka Cristiano Ronaldo kwenye Champions League usiku wa jana

R eal Madrid waliingiza mguu mmoja kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya jana usiku baada ya kupata ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Schalke 04 mjini  Gelsenkirchen.
Usiku wa jana pia, Cristiano Ronaldo na wenzie waliweza kuendelea kuvunja na kuweka rekodi mpya katika michuano hii.
Hapa, najaribu kukueletea takwimu mbalimbali za rekodi walizoweka Madrid na Ronaldo baada ya mchezo wa jana.
25CF680400000578-2959030-image-a-40_1424291046123
76 – Ronaldo sasa ametimiza jumla ya magoli 76 na kuwafikia Lionel Messi na Raul katika michuano yote ya ulaya.
72 – Nahodha huyo wa Ureno anahausika zaidi ya robo ya magoli yote yaliyofungwa na wareno kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya – magoli 72 kati ya 274.
58 – Goli la Ronaldo jana usiku lilikuwa goli la 58 katika Champions League –  akiwa amevalia jezi za Real Madrid.
25CF687B00000578-2959030-image-a-110_1424295782236
29 – Mpaka kufikia usiku wa jana Ronaldo anaongoza kwa magoli na assists kwa misimu miwili katika michuano hiyo ya ulaya. Ukiunganisha magoli na assists Ronaldo anaongoza kwa umbali mrefu – akiwa na jumla ya magoli + assists 29 – huku anayemfuatia Lionel Messi akiwa na 18.
28 – Ushindi wa jana usiku umemfanya Ronaldo atimize idadi ya ushindi katika mechi 28 za champions league, na kwa kufanya hvyo sasa amewapita Edwin van der Sar na Victor Valdes waliokuwa wakiongoza.
12 – Goli lake la kichwa jana lilikuwa la 12 mfululizo kwa Ronaldo kufunga ugenini katika michuano ya ulaya.
10 – Ushindi wa 2-0 dhidi ya vijana wa Roberto di Matteo umeifanya Madrid kushinda mara 10 mfululizo katika Champions League.
6 – Ronaldo ni mchezaji pekee wa sita kuweza kufunga magoli 10 au zaidi ya kichwa katika michuano ya ulaya. Anaungana na Fernando Morientes, Raul, Inzaghi, Jardel na Andriy Shevchenko katika listi hiyo

No comments:

Post a Comment