Samatta alishindwa kujiunga na CSK Moscow wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka huu kutokana na kupata majeraha
WAKALA wa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe, Jamal Kasongo
amesema, amefanya mazungumzo na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi
kujadili juu ya kuuzwa kwa Samatta barani Ulaya.
Kasongo ameiambia Goal, mazungumzo kuhusu
mshambuliaji huyo kuuzwa kwenye majira ya kiangazi ni mkubwa kutokana na
mmiliki huyo wa TP Mazembe kuridhia kwasababu anaweza kupoteza pesa
nyingi endapo atakataa na Samatta anamaliza mkataba wake wa kuichezea
timu hiyo Aprili 2016.
“Katumbi ameridhia baada ya hivi karibuni kukutana naye na kuzungumza
kuhusu mstakabali wa Mbwana Samatta na huu ndiyo muda pekee kwa Katumbi
kutengeneza pesa ni majira ya kiangazi mwaka huu au majira ya baridi
mwezi Januari mwakani, akishindwa hapo mwezi wa nne mwakani Mbwana
atakuwa mchezaji huru, ataondoka bure,”amesema Katumbi.
Samatta alishindwa kujiunga na CSK Moscow wakati wa dirisha dogo la
usajili mwezi Januari mwaka huu kutokana na kupata majeraha siku moja
kabla ya kucheza mechi ya kirafiki ambayo maamuzi yangetoka moja kwa
moja katika siku tatu alizofanya majaribio CSK Moscow alicheza vizuri na
alifunga magoli matatu lakini alishindwa kucheza mechi ya kirafiki
baada ya kuumia kifundo cha mguu.
No comments:
Post a Comment