WAKATI Waganda Joseph Owino na Dan Sserunkuma wakiropoka yao baada
ya kutemeshwa kazi Simba, kiungo mahiri wa klabu hiyo, Said Ndemla
ameikata maini Yanga iliyokuwa inamnyatia kwa kumwaga wino mkataba wa
miaka miwili.
Taarifa za ndani za Simba zinasema kuwa, Ndemla
amesaini mkataba huo jana mchana na kulipwa kiasi cha Sh40 milioni
pamoja na gari ili kumtuliza mzuka baada ya kuenea kwa habari kwamba
Yanga walikuwa tayari kumalizana na mchezaji huyo chipukizi.
Inaelezwa kuwa Kamati ya Usajili ya Simba
ililazimika kumaliza mambo mapema kwa kuhofia kuzidiwa ujanja na Yanga
ambayo imekuwa ikimmezea mate kiungo huyo, ambaye tangu apatishwe katika
kikosi cha wakubwa toka timu ya vijana amekuwa gumzo kwa soka lake.
No comments:
Post a Comment