Pluijm amesema watatumia mechi za ligi ya Vodacom
kujiandaa na mchezo huo wa marudiano ambao anajua utakuwa mgumu kutokana
na kucheza ugenini
BAADA ya ushindi wa mabao 5-1 walioupata jana kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho Afrika kocha wa Yanga Hans van der Pluijm, amesema
matokeo hayo hayawapi muda wa kupumzika kwani bado wanakazi kubwa ya
kuhakikisha wanamaliza vizuri dakika 90 za Zimbabwe.
Pluijm ameiambia Goal, wapinzani wao FC Platinum, ni
timu nzuri na wanalazimika kucheza kwa umakini mkubwa kwenye mchezo wa
marudiano utakaopigwa April 3 kwenye dimba la Mandava Zimbabwe.
“Niushindi mzuri lakini hatupaswi kuridhika nao tunapaswa kuendelea
kujituma kwa kurekebisha mapungufu ambayo yamejitokeza na tutakapokwenda
Zimbabwe tulinde ushindi wetu kwa kushambulia zaidi na siyo kuzuia kwa
sababu wapinzani wetu FC Platinum ni wazuri,”amesema Pluijm
Pluijm amesema watatumia mechi za ligi ya Vodacom kujiandaa na mchezo
huo wa marudiano ambao anajua utakuwa mgumu kutokana na kucheza ugenini
na wapinzani wao nao wanahitaji kuwaonyesha kuwa wanaweza hivyo
wanahitaji kufanya kazi ya ziada.
No comments:
Post a Comment