Thursday, 11 June 2015

Mohamed Hussein, Ngasa na Msuva kukabidhiwa zawadi tarehe 11

Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, nibaadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.

Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.
Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Vodacom watatoa zawadi kwa bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :
1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
i. Mohamed Hussein (Simba SC)
ii. Mrisho Ngasa (Young Africans)
iii. Saimon Msuva (Young Africans)
2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
i. Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
ii. Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
iii. Shaban Hassan (Coastal union)
3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
i. Goran Kopunovic (Simba SC)
ii. Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
iii. Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)
4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
i. Israel Mjuni Nkongo
ii. Jonesia Rukyaa
iii. Samwel Mpenzu
5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
i. Mgambo JKT
ii. Mtibwa Sugar
iii. Simba SC

No comments:

Post a Comment