Katika mchezo huo Ajib alionyesha kiwango cha juu kwa kuwasumbua mabeki wa Yanga na mara kadhaa alijaribu kupiga mashuti
MSHAMBULIAJI anayekuja kwa kasi wa Simba Ibrahim Ajibu, ameibuka mchezaji bora katika mechi za wiki hii kupitia mtandao wa Goal.com baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika mechi ya wataji wa jadi Simba na Yanga.
Katika mchezo huo Ajib alionyesha kiwango cha juu kwa kuwasumbua mabeki wa Yanga na mara kadhaa alijaribu kupiga mashuti lakini bahati haikuwa upande wake kama ilivyokuwa Jumamosi iliyopita alipofunga mabao 3 peke yake hat-trick dhidi ya Tanzania Prisons.
Pamoja na kupambana na mabeki wenye majina makubwa mshambuliaji huyo aliyepandishwa kucheza timu ya wakubwa msimu huu akitokea Simba B, amekuwa na akitoa mchango mkubwa kwa kikosi cha Simba hasa katika ufungaji wa mabao na kwasasa anashika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji.
Ajibu aliyepania kuifunga Yanga jana amesema licha ya kushindwa kutimiza ndoto zake ataendelea kujifua ili aweze kufanya hivyo siku nyingine watakapokutana na Yanga.
Tangu alipoanza kuichezea Simba Ajibu ameshaifungia Simba hat- trick mbili moja ikiwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na nyingine kwenye ligi kuu Tanznaia bara dhidi ya Tanzania Prisons.