Mbali na kutaka kulipa kisasi lakini pia Yanga ambao
ni wawakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa watataka kushinda
mchezo huo ili kurudi kileleni mwa ligi kuu
MABINGWA mara 24 wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara Yanga kesho
Jumatano watashuka kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam kuwaalika Kagera
Sugar ya Bukoba.
Yanga inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na
pointi 31, itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kulipa kisasi
cha kufungwa bao 1-0, na Kagera katika mchezo wa awamu ya kwanza
uliofanyika kwenye dimba la Kaitaba Novemba 2014.
Mbali na kutaka kulipa kisasi lakini pia Yanga ambao ni wawakilishi
pekee kwenye michuano ya kimataifa watataka kushinda mchezo huo ili
kurudi kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuzidiwa na wapinzani wao Azam
kwa pointi mbili lakini wakiwa nyuma kwa mchezo mmoja.
Kabla ya kufungwa na Simba wiki mbili zilizopita kikosi cha Yanga
kiweza kushinda mechi tatu mfululizo kikiwa ugenini kwenye viwanja wa
vya Mkwakwani Tanga walipoifunga Coastal Union na kisha kuchukua pointi
sita kwenye uwanja wa sokoine Mbeya kwa kuzifunga Tanzania Prisons na
Mbeya City.
Pamoja na kuvurugiwa na Simba kwa kufungwa bao 1-0 Machi 8, niwazi
Yanga wataingia kwa kasi kutaka kuifunga Kagera Sugar na kurudisha
heshima yao ikiwemo kuendeleza furaha iliyowapa mashabiki wake wikiendi
iliyopita kwa kuifunga FC Platinum ya Zimbabwe mabao 5-1, ukiwa ni
mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika CAF.
Kocha Hans van der Pluijm, hakuwepo kwenye timu wakati timu yake
inafungwa bao 1-0 na Kageral lakini kurejea kwake kwenye kikosi cha
Yanga niwazi kumeonyesha mabadiliko na atahakikisha vijana wake
wanapambana kupata pointi tatu ili kujipa matumaini ya kufanya vizuri
kwenye mechi zijazo.
Pluijm ameiambia Goal anaiheshumu Kagera Sugar inayonolewa na kocha
Mganda Jackson Mayanja, lakini akasema pamoja na heshima hiyo amekiagiza
kikosi chake pointi tatu katika mchezo huo ili kuweka mazingira mazuri
ya ubinga.
“Tupo katika ari ya juu kuhakikisha tunaendeleza wimbi la ushindi
tulioupata Jumapili kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum, najua Kagera ni
timu nzuri iliwafunga Simba uwanja wa taifa lakini tumejiandaa
kuhakikisha tunapambana na kupata ushindi kabla ya kwenda Tanga, amesema
Pluijm.
Naye kocha Jackson Mayanja amesema anajitambia vijana wenye umri
mdogo na viwango vya juu kwenye kikosi chake hivyo hatishiki anachojua
amekuja Dar es Salaam kuchukua pointi tatu kama alivyofanya kwenye
mchezo wa kwanza.
Kwenye msimamo wa ligi Kagera inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi
25 na katika pambano lake lililopita dhidi ya Coastal Union ili
ilazimisha sare ya 2-2.
“Tunamatumaini ya kuifunga Yanga tupo vizuri vijana wote wapo sawa na
tunacho subiri ni muda wa mchezo ili tuweze kuchukua kilichotuleta Dar
es Salaam ,”amesema Mayanja.
No comments:
Post a Comment