Tuesday 17 March 2015

Nooij atangaza kikosi cha Taifa Stars

KOCHA ‘Taifa Stars’ Mart Nooj, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mart Nooj, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaopigwa Machi 29 uwanja wa CCM Kirumba jijin Mwanza.
Kikosi cha Stars kinatarajia kuingia kambini machi 22 machi katika hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea jijini Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo.
Wachezaji walioitwa na kocha Mart Nooij kujiandaa na mchezo huo ni; Magolikipa, Deogratius Munish, Aishi Manula na Mwadini Ali.
Mabeki ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salim Mbonde, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua,Abdi Banda na Hassan Isihaka.
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Haroun Chanongo na Mwinyi Kazimoto.
Washambuliaji ni Saimon Msuva , Mrisho Ngasa, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, John Bocco, na Juma Luizio.
Wapinzani wa Stars Malawi wanatarajiwa kuwasili Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.

No comments:

Post a Comment