Yanga
imerejea kileleni Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0.
Ushindi huo
umeifanya Yanga kufikisha pointi 28 dhidi ya Azam FC yenye 26 ambayo
imelazimishwa sare ya bila mabao dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Yanga imebuka
na ushindi huo mnono kwenye Uwanja wa ugenini wa Sokoine jijini Mbeya ikiwa ni
baada ya viungo wake Simon Msuva na Andrey Coutinho kufunga.
Msuva
amepachika mabao mawili, huku Coutinho na kukamilisha idadi ya tatu bila dhidi
ya kikosi cha David Mwamwaja ambaye alitamba leo ingekuwa kazi ngumu kwa Yanga.
Pamoja na
kuwa ugenini, Yanga walitawala mchezo kwa vipindi vyote huku wakipoteza nafasi
nyingi za kufunga.
Mara kadhaa,
Prisons nao walijitutumua hata hivyo kwa dakika zote 90 walifanikiwa kufanya
mashambulizi makali au makubwa matatu tu.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wamekubali kuipisha Yanga kileleni.
Azam
FC imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, Pwani.
Sare
hiyo ya bila mabao, inaifanya Azam FC kufikisha pointi 26 wakati Yanga
ambayo imeibuka na ushindi dhidi ya Prisons inafikisha pointi 28.
Azam FC ndiyo inaongoza kwa kuwa na pointi 25 sawa na Yanga lakini tofauti ilikuwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika
kipindi cha kwanza dakika 15 za kwanza, Azam FC ilishambulia zaidi,
lakini washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche hawakuwa makini.
Kipindi
cha pili, mambo yalibadilika na Ruvu Shooting kutawala huku wakionekana
kuwasumbua Azam FC, hata hivyo nao hawakuwa makini kumalizia nafasi
walizozipata.
No comments:
Post a Comment