Wednesday, 18 February 2015

DEWJI AWAAMBIA SIMBA INAHITAJI UTULIVU KUTENGENEZA MAMBO BORA


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema kikosi cha timu yao ni bora lakini kuna mambo kadhaa ya kufanya na wanachama na mashabiki wanahitaji utulivu.



Dewji amesema wakati uongozi wa sasa unaingia madarakani, Simba haikuwa katika kiwango kizuri kwa zaidi ya miaka miwili nyuma.

"Tunalazimika kutengeneza timu, kufanya mabadiliko na wakati huo huo kuna presha ya kutaka kushinda.

"Ninaamini kutakuwa na mabadiliko makubwa katika mzunguko wa pili. Lakini wanachama na mashabiki, wavute subira kidogo.

"Utaona timu inaanza kuimarika, hata uchezaji wake si kama mechi nne tano zilizopita. Pia wakumbuke tuna kocha mpya na ndiyo anaanza kuzoea kwa kuwa hana hata mechi sita za Ligi Kuu Bara," alisema.

Katika siku za hivi karibuni, Dewji amekuwa akionekana kuwa karibu na timu zaidi na alionekana na kikosi hicho mjini Morogoro, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Moro

No comments:

Post a Comment