SIMONI Msuva ndiye mchezaji bora wa Ligi ya Vodacom
Tanzania bara msimu wa 2014/15 lakini unamjua vizuri mshindi huyo wa
tuzo mbili?
SIMONI Msuva ndiye mchezaji bora wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara
msimu wa 2014/15 lakini unamjua vizuri mshindi huyo wa tuzo mbili
nyingine ikiwa ni ya ufungaji bora sehemu alizopitia hadi kufika hapo?
Msuva amechangia Ubingwa wa Yanga kwa Asilimia 75
Msuva aliyechangia asilimia 75 ya ubingwa wa Yanga msimu uliopita kwa
mabao yake 17 pamoja na kutoa pasi za mwisho 12 ambazo zilizaa mabao
Aliwahi jaribu Bahati katika muziki
Amepitia mahangaiko mengi ikiwemo fani ya uchezaji muziki kabla ya
kugeukia katika soka. Awali mwanzoni mwa miaka ya 2010 kinda huyo
aliwahi kuwa ni mmoja wa vijana wanaojifundisha muziki kwenye kundi la
kulea vipaji la Tanzania House of Talent THT, na kuonekana kwenye kumbi
mbalimbali za burudani akiwa ni densa wakati wasanii wakubwa wa kundi
hilo wakutoa burudani.
Lakini baada ya miaka kadhaa ya kukaa kwenye kundi hilo pasipo kupata
mafanikio aliona nivyema akatafuta fani nyingine ambayo inaweza kumtoa
kimaisha ndipo alipogeukia katika mchezo wa soka na moja kwa moja
akajiunga kwenye kituo cha kukuza vipaji vya vijana wadogo kiitwacho
Wakati Ujao.
Anaongoza kwa staili nyingi za kushangilia
Msuva anayeongoza kwa kuwa na staili nyingi za ushangiliaji pindi anapofunga magoli
Aliwahi kuchezea Azam
aliwahi kuchukuliwa na kituo cha kuleleza vijana cha Azam ambacho
baadaye kilimuacha na mchezaji huyo akasajiliwa na timu ya Moro United
ambayo hata hivyo haikudumu kwenye ligi ya Vodacom na mwishoni mwa msimu
ilishuka na kuwa mchezaji huru.
Alisajiliwa na Yanga msimu wa 2011/12
Msimu uliofuata wa 2011/12 nyota huyo akasajiliwa na Yanga hapo ndipo
mafanikio ya mchezaji huyo yalipoanza kuonekana kwa kuanza kufanya
vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za magoli kwa timu yake licha ya
kuonyesha mapungufu kadhaa mwanzoni mwa msimu kwa kuwa mbinafsi na
kushindwa kutengeneza nafasi kwa wenzake.
No comments:
Post a Comment