Thursday 22 January 2015

Stand United na Ruvi Shooting zimetoa wachezaji wawili kila moja

1.Abdallah Rashid kipa chipukizi wa Ruvu Shooting ambaye katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga alionyesha kiwango cha Juu na kuwa kikwazo cha timu hiyo kukosa ushindi kutokana na kuokoa mashambulizi mengi kwenye lango lake.
Kutokana na uhodari aliouonyesha kipa huyo na kuipa pointi moja Ruvu Shooting Rashid anapata alama 1.
2.Michael Aidan huyo ni beki wa kushoto wa Ruvu Shooting ambaye pia alingara kwenye mchezo wa Jumamosi wakati timu yake ikipambana na Yanga.
Katika mchezo huo Michael Aidan alionyesha uwezo mkubwa na kuongeza safu ya mashambulizi kwenye lango la wapinzani wao anapata 2.
3.Edward Charles beki chipukizi wa klabu ya Yanga ambaye kocha Hans van der Pluijm ameonyesha kumuamini na kumpa nafasi kwenye kikosi chake cha kwanza.
Katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting Charls alionyesha kiwango cha juu na kuwavutia watu wengi anapata 3.
4.Idd Mobi beki namba nne wa Stand United ya Shinyanga ni mmoja wa mabeki wanaochipukiza kwa kasi msimu huu kwani ameweza kuwadhibiti washambuliaji hatari akiwemo Emmanuel Okwi na Didier Kavumbagu.
Kutokana na msimu huu kuwa ndiyo wa kwanza kwa mchezaji huyo kucheza Ligi Kuu anapata alama 4 kwa sababu ni mmoja wa mabeki waliofanya kazi kubwa Jumamosi licha ya timu yake kupoteza mchezo kwa kufungwa 1-0 na Azam.
5.Rajabu Zahiri beki namba tano wa Yanga ambeye alitumiwa na kocha Hans van der Pluijm kuziba nafasi ya nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting Rajabu Zahiri alionyesha uwezo mkubwa akishirikiana vyema na mkongwe Kelvin Yondani anapata alama 5
6.Daud Jumanne huyu ni kiungo mkabaji wa Kagera Sugar ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kupunguza kasi ya mashambulizi kwenye lango la timu yake na kuiweka Kagera kwenye nafasi nzuri hadi sasa.
Daudi Jumanne amekuwa akitimiza vyema majukumu anayopewa na kocha wake Jackson Mayanja licha ya kupoteza mchezo Jumamosi lakini kiungo huyo alitoa msada wa kutosha anapata 6.
7.Haruna Chanongo huyu ni winga wa Stand Unite ambaye amejiunga kwa mkopo wa miezi sita akitokea Simba na amekuwa na mchango mkubwa tangu alipo tuwa timu hiyo .
Chanongo ameweza kuisaidia Stand United kutoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar na baadaye Polisi Moro wakiwa ugenini na licha ya kupoteza mechi dhidi ya JKT Ruvu na Azam lakini ametoa msaada mkubwa kwa timu hiyo anapata alama 7.
8. Frank Domayo Kiungo wa Azam FC ambaye ameingia kwa mara ya kwanza kwenye team of the week ya Goal hiyo na Jumamosi ilikuwa ni mechi yake ya kwanza kwenye ligi na kuonyesha kiwango cha juu kilicho mvutia kila mmoja.
Licha ya kuwa huo ndio ilikua mechi yake ya kwanza lakini Domayo ndiye mfungaji wa bao pekee lililoipa pointi tatu Azam FC na kupaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanznaia bara anapata 8.
9.Danny Sserunkuma mshambuliaji mpya wa Simba ambaye amesajiliwa kwenye dirisha dogo akitokea Gor Mahia ya Kenya baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi Jumamosi alizinduka na kuonyesha kiwango cha juu.
Bao lake alilofunga dakika ya 26 ndilo lililofufua matumaini ya Simba kupata ushindi katika mchezo huo wa ugenini ambao uliifanya timu hiyo kupaa hadi nafasi ya tisa ikiwa na pointi 12 anapata alama 9.
10. Amme Ali Huyu ni mshambuliaji hatari wa Mtibwa Sugar ambaye msimu huu amekuwa moto wa kuotea mbali kutokana na kiwango ambacho anakionyesha.
Amme Ali aliifungia Mtibwa Sugar bao la kusawazisha Jumapili wakati timu hiyo ilipopambana na JKT Ruvu kwenye uwanja wa Azam Complex Chamaz anapata 10.
11.Brian Majwega huyu ni winga wa pembeni wa Azam ujio wake kwenye kikosi chaAzam umejionyesha dhahiri kutokana na kazi anayoifanya kwenye kikosi hicho.
Pamoja na kwamba bado hajaifungia timu hiyo bao lakini amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuwatengenezea nafasi washambuliaji Didier Kavumbagu na Kipre Tchetche anapata 11.

No comments:

Post a Comment