Thursday 8 January 2015

MNYAMA SIMBA USO KWA USO NA POLISI NUSU FAINALI Z’NZIBAR

SAM_4389MABINGWA watetezi wa kombe la Mapinduzi, KCC ya Uganda wamevuliwa rasmi ubingwa wao kufuatia kufungwa penalty 5-4 na Maafande wa Polisi Zanzibar katika mchezo wa robo fainali ya pili ya kombe hilo uliomalizika jioni hii uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshindi wa mechi hiyo amelazimika kupatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya timu zote kutoka suluhu ndani ya dakika 90.
Katika mikwaju mitano ya kwanza, timu zote zilifunga mitatu na kukosa miwili.
Penati ya sita,  timu zote zilipata ambapo kwa upande wa Polisi aliyefunga mkwaju huo ni Mohammed Salim na kwa upande wa KCC alifunga Kasule Owen. 
Ally Khalid wa Polisi alifunga penati ya saba, wakati, Saimon Namwanja wa KCC alikosa penalti ya saba na kuilaza njaa timu yake.
Kwa ujumla penalti 14 zimepigwa katika robo fainali ya kwanza.
Dhahiri bahati haikuwa upande wa KCC kwani walitengeneza nafasi nyingi katika vipindi vyote viwili, lakini washambuliaji wake walishindwa kuzibadili kuwa magoli.
SAM_4394
Penati ya sita,  timu zote zilipata, lakini penati ya saba Polisi walipata na KCC wakakosa na kufanya jumla ya penalti 14 kupigwa katika mchezo huo.
Dhahiri bahati haikuwa upande wa KCC kwani walitengeneza nafasi nyingi katika vipindi vyote viwili, lakini washambuliaji wake walishindwa kuzibadili kuwa magoli.
Waliofunga penalti kwa upande wa Polisi ni  Daniel Joram, Mohammed Seif, Abadallah Mwalimu, Mohammed Salim na Ally Khalid, wakati waliokosa ni Suleiman Makungu na Juma Ally.
Waliofunga penalti kwa upande wa KCC ni Tom Masiko, Ronnie Kiseka, Saka Mpima, Kasule Owen, wakati wachezaji waliokosa ni Ivan Ntege, Wadri Willium na Saimon Namwanja.
Wakati huo huo, kamati ya mashindano ilimtangaza Tom Masiko wa KCC kuwa mchezaji bora wa mechi ya leo na alipewa zawadi ya king’amuzi cha Azam TV.
Kwa matokeo haya, Polisi Zanzibar itakutana na Simba katika mechi ya nusu fainali ya kwanza itakayopigwa januari 10 mwaka huu.
Mechi nyingine ya robo fainali inaendelea muda huu baina ya Azam fc na Mtibwa Sugar, wakati majira ya saa 2:15 usiku Yanga watachuana na JKU katika robo fainali ya mwisho

No comments:

Post a Comment