Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano wa Yanga Jerry Murro akizungumza na waandishi wa habari leo
mjini Unguja katika kambi ya timu yao iliyopo hoteli ya Zanzibar Ocean
View
KLABU ya Yanga imetengaza rasmi
kuachana na mlinda mlango wake Juma Kaseja kwa madai kuwa Tanzania One
huyo wa zamani hajaonekana klabuni kwa majuma matatu.
Mkuu wa Idara ya habari na
Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amekutana na waandishi wa habari leo
mjini Zanzibar na kueleza kuwa kitendo hicho cha Kaseja kimemfanya
avunje mwenyewe mkataba wake na klabu hiyo yenye maskani yake makutano
ya Twiga na Jangwani , Kariakoo, Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment